has gloss | swa: Neptune ni sayari kubwa katika mfumo wa jua, ya nane kutoka katika jua na ya nne kwa ukubwa wa kipenyo. Neptune hukaa karibia muda wote katika umbali ambao haubadiliki kutoka kwenye jua. Umbali wa takribani kilometa bilioni 4.5 (sawa na maili bilioni 2.8) kutoka katika jua. Obiti ya Neptune inakaribia kufikia duara kamili (obiti nyingi za sayari huwa ni duara paba). Wanaanga wanaamini kuwa, kwa ndani katikati Neptune imeundwa na miamba ambayo inazungukwa na kiwango kikubwa cha maji iliyochanganyika na vitu vyenye asili ya miamba. Kutoka ndani kabisa, maji haya yametawanyika kuelekea juu mpaka ilipokutana na tabaka la hewa liloundwa na hydrogen, helium na kiwango kidogo cha gesi ya methane. Neptune ina bangili nne na miezi kumi na moja inayofahamika hadi sasa. Ingawa ujazo wa Neptune ni mara 72 ya ule ujazo wa dunia, tungamo lake ni mara 17 tu ya lile la dunia. Kutokana na ukubwa wake, wanasayansi wameiweka Neptune, pamoja na sayari zingine Jupiter, Saturn na Uranus katika kundi la sayari kubwa kabisa zinazofahamika kama Jovian planets. |